MAKAMU Mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange Kaburu amesema wapo kwenye hatua za mwisho za kupata saini ya beki wa APR, Mbuyu Twite kuziba pengo la Kelvin Yondani aliyetimkia Yanga.Akizungumza na gazati hili jana, Kaburu alisema mpango wao wa kuimarisha kikosi chao unakwenda vizuri na umepata baraka zote za kocha Milovan Circkovic.
Alisema beki huyo amekubali kucheza Simba msimu ujao."Ni mapema kutaja kiasi cha fedha tutakachotumia kukamilisha usajili wake, lakini wiki ijayo atatua nchi kwa lengo la kukamilisha usajili." alisema Kaburu.
Akithibitisha hilo kwa simu jana kutoka Kigali, Rwanda,Twite alisema kuwa anashawishika kuja kukipiga Simba baada ya viongozi wa klabu hiyo kuzungumza naye.
"Ukweli ni kwamba jana (juzi) kabla hatujarudi nyumbani Rwanda nilikutana na watu wa Simba tukazungumza ili nije kuichezea timu yao, niliwaambia nipo tayari ingawa hatukufikia muafaka wa moja kwa moja.
"Hata hivyo, hakuna shaka kwamba mambo yatakwenda vizuri na hatutashindwana kwa vile binafsi napenda kuja kucheza Tanzania," alisema Twite
"Hata hivyo, hakuna shaka kwamba mambo yatakwenda vizuri na hatutashindwana kwa vile binafsi napenda kuja kucheza Tanzania," alisema Twite
Kuhusu dau analohitahi ili aweze kujiunga na Simba,Twite hakuwa tayari kusema.
Katika hatua nyingine, Kaburu alisema kabla ya kocha Milovan kuondoka alishauri kuachwa kwa beki Lino Musomba, Haruna Shamte pamoja na Shabaan Kinje.
Katika hatua nyingine, Kaburu alisema kabla ya kocha Milovan kuondoka alishauri kuachwa kwa beki Lino Musomba, Haruna Shamte pamoja na Shabaan Kinje.
"Kocha ameonyesha kutoridhisha na viwango vya wachezaji hao hivyo ameshauri tuwaache," alisema na kuongeza:
"Musomba alionekana kama hayuko tayari kucheza, naye Shamte ameshindwa kuonyesha kiwango hivyo ametushauri kuwaacha.
"Musomba alionekana kama hayuko tayari kucheza, naye Shamte ameshindwa kuonyesha kiwango hivyo ametushauri kuwaacha.
Kuhusu ushiriki wa Simba kwenye michuano ya Kombe la BancABC Supa 8, kiongozi huyo alisema hawatashiriki kutokana na maslahi duni.
Kaburu alisema katika mkataba uliongia kati ya TFF na wadhamini wa michuano hiyo unaonyesha shirikisho lilitapokea asilimia 50."Sisi kama wadau wakubwa wa mashindano hayo tulipaswa kushirikishwa tangu mwanzo ili tufaidike kuliko ilivyokuwa sasa."
Ukiangalia mkataba huo utaona kila timu inapewa Sh5 milioni za maandalizi, na zawadi anapewa bingwa pekee ambayo ni Sh30 milioni."Hakuna zawadi ya mshindi wa pili, watatu sasa hayo ni mashindano gani, hatutoshiriki na endapo tutaamua kucheza basi tutaitumia timu ya vijana chini ya miaka 20.
Chanzo:http://www.mwananchi.co.tz
0 comments:
Post a Comment