KATIKATI ya mwaka jana, dunia ilishuhudia harusi ya mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba, raia wa Ivory Coast aliyemuoa mwanadada, Lala Diakite.
Wawili hawa walikuwa na mahusiano ya muda mrefu lakini wameoana na sasa wamekuwa mwili mmoja, ni mke na mume kamili.
Katika harusi ile, wachezaji wote wa Chelsea walialikwa kwenye hafla hiyo pamoja na marafiki zake kama wachezaji wachezaji wa Manchester City, Kolo Toure na Yaya Toure. Drogba pia alimwalika Emmanuel Eboue wa Arsenal na Ivory Coast kujumuika naye katika hafla hiyo iliyokuwa ya kipekee.
Lala ni mpenzi wa Drogba tangu alipokuwa akichezea Marseille nchini Ufaransa. Mara zote, Lala alikuwa karibu sana na Drogba tangu alipokuwa mchezaji wa kawaida hadi kuwa mchezaji maarufu duniani. Kwa kweli Drogba na Lala wanapendana sana.
Lakini hivi karibuni, kulikuwa na habari kuwa mke wa kipa wa zamani wa Ghana, Richard Kingstone alitoa mpya kwa kusema ilibidi atumie 'juju' kumfifisha mumewe ambaye ni kipa wa Ghana ili arudi nyumbani.
Ni kawaida kwa mke kumtakia mema mumewe lakini hii ya mke wa Kingstone ni ya aina yake.
Mke huyo alipohojiwa katika kipindi kimoja cha mahojiano katika TV ya Ghana, alikirio kusema kuwa amefanya kila njia ya ulozi kumharibia mume wake ashuke kiwango ili arudi nyumbani wakae pamoja.
Richard Kingson, 34, alikuwa akichezea klabu kubwa za Ligi Kuu ya England ikiwemo Birmingham, Wigan na Blackpool na alikuwa kipa mahiri katika timu yake ya taifa ya Ghana.
Lakini tangu kuachwa na Blackpool mwaka jana, hadi leo hajapata timu na amekuwa akihaha bila mafanikio.
Sasa, mke wake, Adelaide Tawiah alionekana kwenye Televisheni ya Nigeria akisema kuwa ametumia nguvu nyingi za giza kumharibia mume wake asiendelee kuwika ili arudi nyumbani.
Anasema: “Najuta kumharibia maisha Richard tangu tulipooana. Nilitumia nguvu nyingi za giza kumharibia arudi, lakini sasa ndiyo nimeharibu kila kitu.
“Nilikuwa nafanya mambo haya sana, na hata nilimfunga kiasi kwamba hata hawezi kufanya mapenzi na mimi.”
Hatua yake imekuja baada ya maswali kadhjaa kwenye TV katika kipndi cha 'Roho ya Ushetani' kinachorushwa na televisheni ya Nigeria.
Richard, alioyemuoa Adelaide baada ya Fainali za Kombe la Dunia 2010, alisema kupitia mtandao wa Kijamii wa Facebook akisisitiza: “Mke wangu siyo mchawi.”
Anasema: "Watu wana dhana mbaya na mke wangu “imani potofu”.
Hata wiki iliyopita, Adelaide alikataa akidai kuwa yeye si mchawi isipokuwa ni roho tu iliyotamka maneno hayo huku akidai hakumbuki hata kilichotokea.
Anasema: “Sikumbuki...sikumbuki hata kilichotokea."
“Mimi siyo mchawi kama ilivyokuwa imevumishwa. Mume wangu anafahamu jinsi ninavyompa moyo aweze kuendelea kucheza Ulaya.
chanzo:mwananchi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment