Monday, 30 July 2012
YANGA "KULA BATA" WIKI NZIMA!!!
MABINGWA wa mara mbili mfululizo michuano ya Kombe la Kagame, Yanga wanaingia kambini wiki ijayo baada ya mapumziko mafupi kujiandaa na Ligi Kuu, huku Kocha Thomas Saintfiet akiwasifu wachezaji kwa mshikamano na nidhamu kwenye michuano ya Kombe la Kagame.
Yanga ilitwaa taji la Kagame mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kufunga Azam FC mabao 2-0 katika mchezo wa fainali kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kocha Saintfiet, alisema kikosi che kimefanya vizuri kwenye michuano ya Kagame kutokana na nidhamu na kujituma kwa wachezaji.
"Wachezaji wamefanya makubwa kutwaa ubingwa, lakini hili limewezekana kwa sababu ya mshikamano na nidhamu kubwa waliyoonyesha," alisema Saintfiet.
"Naushukuru uongozi mzima wa Yanga pamoja na wachezaji wangu, wote wamekuwa sehemu kubwa ya mchango wa mafaikio tuliyopata," alisema.
Aidha aliongeza kuwa kwa sasa wachezaji wanatakiwa kupumzika kidogo kufuatia kucheza mechi mfululizo kabla ya programu mpya kwa ajili ya Ligi Kuu.
Katibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwesingwa alisema wachezaji hao watarejea kambini wiki ijayo na hawatashiriki michuano ya Super8 kama walivyoombwa na TFF.
"Tumewapa mapumziko ya wiki moja na baada ya maombi ya kocha. Wanahitaji kupumzika kufuatia kucheza mfululizo bila kupumzika," alisema.
chanzo:http://www.mwananchi.co.tz
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment