Pages

Friday, 21 September 2012

KADO AMKALISHA KUTI KAVU KATIBU WA YANGA

KIPA Shaban Hassan ‘Kado’ ambaye anaichezea Mtibwa Sugar kwa mkopo, amezua tafrani kubwa ndani ya timu yake ya Yanga, kwa kumuingiza lawamani Katibu wa Yanga, Selestine Mwesigwa.
Kado ambaye alionyesha kiwango cha juu katika mechi ya juzi dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, aliwashangaza mashabiki wa timu yake hiyo inayommiliki na kuhoji imekuwaje acheze wakati yupo kwa mkopo Mtibwa.
Mashabiki wa Yanga walivamia katika vyumba vya wachezaji wakati wa mapumziko, wakimlalamikia Mwesigwa juu ya uamuzi wa kuruhusu kipa huyo kucheza katika mchezo huo.
Wakiwa na jazba, mashabiki hao walilaani uamuzi huo ingawa Mwesigwa hakuwepo eneo hilo. 
Alipoulizwa baadaye juu ya madai hayo, Mwesigwa alisema katika mkataba wa makubaliano ambayo timu yake iliingia na Mtibwa, hakukuwa na kipengele kinachomzuia kipa huyo kucheza katika mchezo baina ya timu hizo.
“Kado alikuwa na uhalali wa kucheza katika mchezo wa jana (juzi), hakukuwa na kipengele kilichoonyesha kwamba hatatakiwa kucheza endapo timu hizi zitakutana,” alisema Mwesigwa.
chanzo:http://www.globalpublishers.info

0 comments:

Post a Comment