Pages

Tuesday 11 September 2012

MAZUNGUMZO KUWAOKOA SIMBA!!!!


Robert Atah, mkurugenzi wa masuala ya kiufundi katika chama cha soka cha Cameroon, amesema wachezaji na vile vile maafisa wa timu wanastahili kusahau tofauti zao kwa madhumuni ya kuiokoa timu ya taifa ya Indomitable Lions.
Atah amesema hayo baada ya Cameroon kufungwa magoli 2-0 na Cape Verde, katika mechi ya mkondo wa kwanza ya kufuzu kushirikishwa katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013 nchini Afrika Kusini.
Atah alielezea chanzo cha matatizo hayo ni wakati Samuel Eto’o alipofanywa nahodha wa timu, nyakati ambazo nahodha wa zamani, Rigobert Song, alipokuwa bado ni mchezaji wa timu hiyo ya taifa.
"Kuna migogoro mingi ndani ya timu kati ya wachezaji na wasimamizi,” aliielezea BBC.
"Hilo ndio ndilo tatizo kubwa, na ikiwa wanaohusika hawatakuwa na suluhu, basi hatuwezi kutazamia mengi katika soka yetu.
"Njia ya kusonga mbele ni maridhiano – tunawafahamu wanaozozana, tunawajua wenye matatizo.
"Ni wachezaji dhidi ya wachezaji, na wachezaji dhidi ya maafisa wakuu, na kwa hiyo ni lazima kuketi pamoja na kupata suluhu."
Anaamini matatizo mengi ya kikosi hicho yalianza wakati timu ikiongozwa na meneja wa zamani Paul Le Guen, na hasa alipomfanya Eto'o kuwa nahodha.
"Wakati Rigobert Song alipovuliwa unahodha na kukabidhiwa Eto'o, kulikuwa na malalamiko katika kikosi – kati ya wale waliomuunga mkono Eto’o, na wale waliomuunga mkono Song,” alielezea.
"Kuanzia hapo mzozo ulianza miongoni mwa wachezaji, na suluhu bado haijapatikana.
"Kwa hiyo huwezi kutazamia wao kukusanyika pamoja na pasipo kusema “kama tulifanya kosa kwa kumfanya Eto’o nahodha huku Song akiwa bado ni mchezaji katika timu, basi tunakiri makosa yetu, na tungelipenda mtusamehe kwa hilo”.
"Ndio tutaweza kuwa na muelekeo sawa – ikiwa hatutakubali makosa yetu, basi hakutakuwa na ufanisi wowote katika kusonga mbele."
Eto'o alipuuza mwito wa kujiunga na kikosi cha Cameroon katika mechi ya kupambana dhidi ya Cape Verde, kufuatia chama cha soka nchini humo kumpiga marufuku kwa miezi minane, kwa kuhusika na mgomo wa wachezaji wa timu ya taifa mwaka jana.
chanzo:bbc

0 comments:

Post a Comment