UBUTU wa safu ya ulinzi katika kikosi cha Simba, umemfanya kocha mkuu wa timu hiyo, Milovan Cirkovic, aazimie kumrejesha beki kisiki wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Beki huyo alijiunga na Yanga hivi karibuni akitokea Simba, akasaini mkataba wa miaka miwili, lakini bado hatima yake haijajulikana kutokana na kudaiwa kusaini mkataba akiwa ndani ya mkataba mwingine.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Milovan alisema beki huyo bado anahitajika kwenye kikosi chake kinachojiandaa na ligi na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Milovan alisema bado hajaridhishwa na safu ya ulinzi ya kati, inayoongozwa na Paschal Ochieng, Komalmbil Keita na Juma Nyosso.
“Safu zote zipo vizuri, lakini bado kuna tatizo kubwa katika safu ya ulinzi, sijaridhishwa na viwango vyao, inahitaji marekebisho ya haraka kabla ya ligi kuanza.
“Kabla ya kuondoka Yondani, nilihitaji beki mmoja mwenye uwezo atakayesaidiana naye, baadaye alikwenda Yanga na kusababisha safu ya ulinzi kuwa mbovu,” alisema Milovan.
chanzo:http://www.globalpublishers.info
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment