Pages

Monday, 10 September 2012

NIYONZIMA:TUMPE NAFASI KAVUMBAGU.

KIUNGO wa kimataifa wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema mshambuliaji Didier Kavumbagu, anatakiwa apewe muda ili awe fiti.
Kavumbagu alisajiliwa na Yanga msimu huu akitokea katika klabu ya Atletico ya Burundi.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Niyonzima alisema Kavumbagu ni mshambuliaji mzuri na ana uwezo mkubwa uwanjani, hivyo mashabiki wampe muda ili aonyeshe kile ambacho wao wanataka.
Alisema watasaidiana na mshambuliaji huyo kwa kumpa pasi nzuri kwenye mechi za Ligi Kuu Bara, ili afunge mabao yatakayoiwezesha timu hiyo kuwa katika nafasi nzuri.
“Bado tunatakiwa tumpe muda, binafsi naona kama mchezaji siyo mbaya, ni mzuri, cha muhimu ni kusubiri tumuone kwenye ligi lakini pia mimi na wenzangu tutasaidiana kumpa pasi nzuri kwenye ligi ili afunge kwa kuwa itatusaidia wote,” alisema Niyonzima.
Kavumbangu amekuwa akilalamikiwa na baadhi ya mashabiki wa Yanga kutokana na kutoonyesha cheche zake kama ilivyokuwa kwenye michuano ya Kagame iliyomalizika mwezi uliopita.
Raia huyo wa Burundi alijiunga na Yanga mwezi Julai, akiwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Burundi msimu uliopita
chanzo:http://www.globalpublishers.info

0 comments:

Post a Comment