KOCHA Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic, amemtangaza kipa wake Juma Kaseja kuwa ni kipa bora zaidi kwenye kikosi chake kinachoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara na Tanzania kwa ujumla.
Milovan alitoa kauli hiyo juzi mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu ya Bara kati ya timu yake dhidi ya Toto African mchezo ambao Simba ililala kwa bao 1-0.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Milovan raia wa Serbia alisema kwa upande wake, Kaseja ndiye kipa bora zaidi Simba na hapa nchini.
Milovan alisema, ubora na umuhimu wake umeonekana kwenye mechi na Toto baada ya kipa namba mbili wa timu hiyo, Wilbert Mweta, kudaka na kufungwa bao la kizembe.
“Mmeona kilichotokea, kipa kafanya uzembe timu imefungwa, siwezi kusema ni yeye mwenyewe kaifungisha timu kwa kuwa timu inapoteza ikiwa na wachezaji 11 uwanjani, lakini kwangu Kaseja ni kipa bora.
“Namhitaji kwenye kikosi changu, ni bora siyo Simba tu bali nchi nzima.
“Umuhimu wake umethibitika leo hii katika mechi na Toto, tumefungwa bao kutokana na uzembe, angekuwa Kaseja sidhani kama tungefungwa,” alisema Milovan.
Kaseja, katika mechi ya ligi dhidi ya Mtibwa Sugar iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, alishutumiwa kuihujumu timu baada ya kufungwa mabao mawili katika mchezo huo uliomalizika kwa Simba kufungwa mabao 2-0.
chanzo:.globalpublisher
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment