Pages

Monday 10 December 2012

Cecafa yawanyima viatu Ngassa, Bocco


KIUNGO mshambuliaji wa kikosi cha Kilimanjaro Stars, Mrisho Ngassa, amekerwa na kitengo cha takwimu ndani ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), baada ya kumnyima ufungaji bora
Kauli hiyo ya Ngassa inakuja baada ya Cecafa kumtangaza Robert Ssentongo wa Uganda kuwa mfungaji bora katika michuano ya Chalenji iliyomalizika juzi jijini Kampala, Uganda.
 Akizungumza na Championi Jumatatu, Ngassa amesema ameshangazwa na hatua ya Cecafa kumtaja Ssentongo kuwa mfungaji bora wakati ana mabao manne, huku yeye (Ngassa) na John Bocco wakiwa na matano kila mmoja.
“Unajua ukweli halisi ni kwamba Cecafa imembeba Ssentongo, ukifuatilia kwa makini mimi na Bocco ndiyo tulimaliza mashindano tukiwa na mabao mengi ambapo kila mmoja alimaliza kwa kufunga mabao matano lakini ajabu tukasikia jana (juzi) waandaaji wanamtangaza Ssentongo kuwa mfungaji bora,” alisema Ngassa na kuongeza:
“Ukweli ni kwamba siku ambayo tulicheza na Uganda na wakatufunga ndiyo siku ambayo Ssentongo alifikisha mabao matatu na ukijumlisha na lile moja alilofunga jana (juzi) katika fainali, utagundua alikuwa na mabao manne, siyo matano kama walivyodai,” alisema Ngassa
chanzo:globalpublishers

0 comments:

Post a Comment