Pages

Wednesday 5 September 2012

Akuffor ni zaidi ya Bocco, Bahanunzi asema Ngassa!!!

KIUNGO mchezeshaji wa Simba, Mrisho Ngassa, amesema makali aliyonayo mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Daniel Akuffor, ni tofauti na wachezaji wengine aliowahi kucheza nao.
Akuffor, ambaye ni raia wa Ghana, amekuwa na mwanzo mzuri tangu asajiliwe na Wekundu hao ambapo amefanikiwa kufunga katika kila mchezo kwenye michezo mitatu Simba iliyocheza ikiwa Arusha.
Akizungumza na Championi Jumatano, Ngassa amesema amewahi kucheza na washambuliaji John Bocco akiwa na Azam FC lakini pia Said Bahanuzi katika kikosi cha Taifa Stars, lakini Akuffor ameonekana bora zaidi kwa upande wake.
“Nafurahi sasa timu yetu tumeanza kuelewana katika safu ya ushambuliaji na kwa upande wangu Akuffor namuona ni bora kati ya washambuliaji ambao nimewahi kucheza nao kwa sababu, yeye ni mwepesi tofauti na washambuliaji wengine,” alisema Ngassa.
“Nimecheza naye katika michezo mitatu na ameonekana ni mtu ambaye kwa beki mzembe ni rahisi kukufunga na nafurahi kuona na yeye akifurahi kucheza na mimi timu moja, nadhani mashabiki wa Simba watulie, mambo mazuri yanakuja.”
chanzo:http://www.globalpublishers.info

0 comments:

Post a Comment