Pages

Sunday, 16 September 2012

MECHI YA SIMBA, LYON YAINGIZA MIL 67!!!



Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Simba na African Lyon iliyochezwa  (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 67,793,000.
Washabiki 11,505 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Kila timu ilipata sh. 14,603,263.47 wakati asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyokatwa ni sh. 10,341,305.08.
Mgawo mwingine umekwenda kwa msimamizi wa kituo sh. 20,000, posho ya kamishna wa mechi sh. 114,000, mwamuzi wa akiba sh. 70,000, et iti.sh. 3,175,000, vishina kwenye tiketi (attachments) sh. 345,150, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.
Umeme sh. 300,000, ulinzi na usafi uwanjani sh. 2,350,000, Kamati ya Ligi sh. 4,867,754.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,920,652.69, uwanja sh. 4,867,754.49, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,947,101.86, gharama za mchezo sh. 4,867,754.49.
Nayo mechi ya ligi hiyo kati ya Tanzania Prisons na Yanga iliyochezwa jana (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya imeingiza sh. 50,435,000.
chanzo:
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

0 comments:

Post a Comment