Pages

Monday, 17 September 2012

Milovan awaondoa Ochieng, Keita Simba SC

KOCHA Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic, amewaondoa mabeki wake kati, Mkenya, Paschal Ochieng na Komalmbil Keita, raia wa Mali, katika kikosi kinachoshiriki Ligi Kuu Bara.
Mabeki hao walitua hivi karibuni na kila mmoja kusaini mkataba wa miaka miwili, kwa ajili ya kuiboresha safu ya ulinzi ya timu hiyo baada ya Kelvin Yondani kuondoka.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Milovan alisema mabeki hao wanahitaji muda zaidi wa kufanya mazoezi  pamoja na wenzao ili wazoeane kabla ya kuwapa nafasi ya kucheza kwenye kikosi chake.
Milovan alisema anapenda sana kuwatumia wachezaji hao lakini bado wanatakiwa kuzoeana sana.
Alisema kwa sasa anawatumia Juma Said Nyosso na Shomari Kapombe lakini angependa kama ageweza kuwachanganya changanya, Kapombe na Ochieng na Nyosso na Keita.
“Safu yangu ya ulinzi hivi sasa nimeifanyia mabadiliko baada ya kuona inacheza kwa kutoelewana, mwanzo nilikuwa nawapanga Ochieng na Keita.
“Nilifikia uamuzi wa kubadilisha upangaji wangu baada ya mabeki hao kucheza kwa kutoelewana, hivyo wanahitaji muda zaidi wa kukaa pamoja ili wazoeane,” alisema Milovan.
chanzo:http://www.globalpublishers.info

0 comments:

Post a Comment