SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), linatarajia kukabidhi sh milioni 7.3 kwa uongozi wa Hospitali ya Temeke, jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya mapato ya sh 146,640,000 zilizopatikana katika mchezo wa kugombea Ngao ya Jamii kati ya Simba na Azam FC uliopigwa Jumanne wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, fedha hizo ni asilimia 5 ya mapato yote na zitapelekwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya kununulia vifaa mbalimbali.
Wambura alisema mechi hiyo ya Ngao ya Jamii, ambayo ilikuwa maalumu kuashiria ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2012/2013, iliingiza sh 146,640,000 kutokana na mashabiki 26,001 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo, ambayo ilimalizika kwa Simba kushinda mabao 3-2.
Alisema, Sekretarieti ya TFF, inatarajiwa kukutana na uongozi wa Hospitali ya Temeke wakati wowote kuanzia leo, ili kujua mahitaji halisi kabla ya kufanya ununuzi wa vifaa husika.
Aidha Wambura alisema kutokana na mapato hayo, mgawanyo ulikuwa kama ifuatavyo: asilimia 18 Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), sh 22,368,813.56; asilimia 5 ya mchango kusaidia jamii (Hospitali ya Temeke), sh 7,332,000; uwanja, sh 10,148,318.64; Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), sh 4,059,327.46; TFF sh 10,148,318.46; na Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF), sh 5,074,159.32.
Mgawanyo mwingine ni Baraza la Michezo la Taifa (BMT), sh 1,014,831.86; kila timu sh 32,265,025.93; asilimia 10 ya gharama za mchezo sh 10,148,318.64; nauli kwa waamuzi na kamishna sh 80,000; posho ya kujikimu kwa waamuzi na kamishna sh 230,000; posho ya waamuzi 400,000; tiketi sh 4,495,800; maandalizi ya uwanja (pitch), sh 400,000; umeme sh 300,000; usafi na ulinzi uwanjani sh 2,350,000; na Wachina (Beijing Construction), sh 2,000.000.
Mchango wa kusaidia jamii kwenye mechi ya Ngao ya Jamii kuzindua ligi ya msimu uliopita kati ya Yanga na Simba, ulikuwa sh 15,000,000 ambazo zilikwenda Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA), kusaidia uchunguzi wa kansa ya matiti kwa kina mama.
chanzo:http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.

0 comments:
Post a Comment