KIUNGO wa Yanga, Nizar Khalfan, amemfanyia mipango mdogo wake, Razak Khalfan, ya kucheza soka la kulipwa nchini Canada katika klabu ya Vancouver Whitecaps aliyowahi kuichezea ambapo dogo huyo ataondoka siku chache zijazo.
Akizungumza na Championi Jumatano, Razak alisema anatarajia kuondoka wakati wowote kuanzia sasa.
“Kaka yangu Nizar ananifanyia mpango wa kufanikiwa kucheza soka la kulipwa katika klabu aliyowahi kuichezea nchini Canada, Vancouver Whitecaps, ili niende kucheza soka la kulipwa.
“Maandalizi yanakwenda vizuri, mipango bado inaendelea na nitaondoka wakati wowote mara baada ya mchakato kukamilika,” alisema Razak, ambaye kwa sasa anaichezea Coastal Union ya Tanga.
Kinda huyo pia amewahi kuichezea Yanga, ingawa hakuwahi kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza.
chanzo:http://www.globalpublishers.info/
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment