Pages

Tuesday, 25 September 2012

OKWI AKANA KUTOKA NA SINTAH!!!

EMMANUEL Okwi amefunguka na kukana taarifa za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mcheza filamu mahiri nchini, Christina Manongi maarufu kwa jina la Sintah.

Okwi, raia wa Uganda anayekipiga Simba ya Dar es Salaam, amesema hajawahi kufikiria wala kushawishika  kutaka kujenga mahusiano wa kimapenzi na msanii huyo.

Majibu ya Okwi kumkana Sintah, ameyaandika na kuyaposti kwenye ukurasa wake wa tovuti ya kijamii ya Facebook.

Kwa siku za hivi karibuni, imedaiwa kuwa Sintah amekuwa akijinadi kwenye vyombo mbalimbali ya habari na tovuti za kijamii kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na Okwi.

"Sintah ni muongo, sijawahi kuwa na mahusiano naye hata siku moja," alisema Okwi, kinara wa kutingisha kamba wa Wekundu hao wa Msimbazi.

Aliandika hivi: "Mabibi na mabwana, nachukua nafasi hii kuweka sawa uhusiano wangu na Christine Sinta, mengi yameandikwa kwenye vyombo vya habari na mitandano ya kijamii kama blog kuwa tupo pamoja, nasema siyo kweli.

"Naamini mtanielewa, nimekwazika sana, nimejitaidi kupuuza yanayosemwa na sasa naamini ni wakati muafaka kujua ukweli," alisema Okwi.

Ujumbe wake unaendelea: "Sina uhusiano wowote wa kimapenzi na yeye (Sintah) kama anavyodai, na hakuna ukweli wowote kwa anayoyaandika. Nawashukuru wote kwa sapoti yetu, Mungu awabariki."

Wakati Okwi akikana taarifa hizo, mwenyewe Sintah pia amemruka Okwi 'hatua ishirini' na kusema mwanasoka huyo hana sifa ya kutoka na mtu kama yeye.

Alisema: "Okwi siyo mwanaume wa 'type' yangu. Kwa sasa niko nje ya nchi nasaka fedha. Sina muda hata kidogo wa kutoka na mwanaume mshamba kama Okwi."

Aliongeza: "Huyu ni mshamba, kama angekuwa anajiamini baada ya kusikia taarifa angenitafuta na siyo kuniandika kwenye mitandao ya na vyombo vya habari.

"Siwezi kutoka na mcheza mpira, kilichoandikwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ni maoni ya watu kwenye tovuti siwezi kukataza.

"Kama Okwi anahitaji kuongea na mimi, akajisafishe kwanza, lakini ukweli unabaki palepale, siwezi kutoka na footballer."
chanzo:mwananchi

0 comments:

Post a Comment