KOCHA mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba, Milovan Cirkovic, juzi alipiga krosi nzuri zaidi ya wachezaji wake Emmanuel Okwi na Daniel Akuffor.
Akiwa amevaa bukta nyeusi, soksi nyeupe na viatu aina ya Copa Mundial kwenye mazoezi yaliyofanyika katika uwanja wa Kinesi jijini Dar, Milovan alionyesha umahiri mkubwa wa kupiga krosi safi zaidi ya wachezaji hao na wengine.
Kocha huyo raia wa Serbia, aliwafunika nyota hao wakati akitoa maelekezo kwa viungo na washambuliaji wake kuhusu jinsi ya kupiga krosi.
Wakati zoezi hilo linaendelea, wachezaji hao na wengine akina Juma Nyosso walikosea kupiga kwa kuwa walitoa nje.
Baada ya kuwaona wachezaji hao wanakosea, yeye mwenyewe kwa haraka aliomba apige kama mfano, ndiyo akawafunika maprofesheno hao kwa kupiga tatu safi, zote zikifungwa na Haruna Moshi ‘Boban’, Ramadhani Chombo ‘Redondo’ na Abdallah Juma.
chanzo:http://www.globalpublishers.info
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment