Pages

Monday, 8 October 2012

TFF yashindwa kuihukumu Yanga malipo ya Twite

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limesema limeshindwa kutoa adhabu kwa Yanga kutokana na klabu hiyo kuchelewa kuilipa Simba malipo ya beki Mbuyu Twite, kwa kuwa suala hilo halimo kwenye kanuni za soka.
Awali, Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliiagiza Yanga iilipe Simba dola 30,000 (zaidi ya Sh milioni 45) ambazo Twite, raia wa Rwanda alizichukua kabla ya kusaini Jangwani kwa dola 50,000 (75,000).
Beki huyo awali alikuwa akizichezea FC Lupopo ya DR Congo na APR ya Rwanda.
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, ameliambia Championi Jumatatu kuwa, hakuna kipengele chochote katika kanuni za Ligi Kuu Bara kinachoibana Yanga kulipa deni hilo.
Hata hivyo, Osiah ameitahadharisha Yanga kuwa, ni vyema ikalipa fedha hizo ili Twite acheze kwa amani na kuepusha uwezekano wa Simba kumpeleka mahakamani kwa kosa la  utapeli.
“Suala la malipo ya fedha za usajili wa Twite halipo katika kanuni zetu, kilichopo hivi sasa ni Yanga kutumia uungwana kuwalipa Simba kabla hawajachukua uamuzi mwingine.
“Ikumbukwe kuwa Simba na beki huyo walipeana fedha hizo mitaani na hata mikataba yao haipo, suala hilo linaweza kuchukuliwa kama hatia kama timu hiyo itamshtaki Twite. Ni vyema ikalipa ili mchezaji huyo acheze mpira,” alisema Osiah.
chanzo:http://www.globalpublishers.info

0 comments:

Post a Comment