Pages

Monday, 1 October 2012

Milovan: Tutawafunga Yanga bila Maftah, Okwi

KOCHA Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic, amesema timu yake itaibuka na ushindi dhidi ya Yanga bila ya wachezaji wawili tegemeo, beki Amir Maftah na kiungo mshambuliaji, Emmanuel Okwi.
Wachezaji hao wanatarajiwa kuukosa mchezo huo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu.
Maftah alipata kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Prisons juzi, wakati Okwi alipata kadi hiyo dhidi ya JKT Ruvu wiki kadhaa zilizopita.
Akizungumza na gazeti hili, Milovan alisema bado ana wachezaji wazuri wenye uwezo mkubwa wa kucheza nafasi za nyota wake hao.
“Ninaomba kuwaondoa hofu mashabiki na wapenzi wa Simba, kwamba tutawafunga Yanga hata bila ya Maftah na Okwi, bado nina wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kucheza nafasi hizo.
“Nataka kuwaonyesha kuwa Simba ni timu kubwa kwa kuwafunga bila ya uwepo wa Maftah na Okwi. Nitatumia siku hizi chache kwa ajili ya kuziboresha nafasi zenye upungufu,” alisema Milovan.
Simba inakwenda kwenye mchezo huo ikiwa kileleni baada ya kushinda mechi zake zote nne za kwanza, wakati Yanga kabla ya mchezo wa jana, ilikuwa imeshinda mechi moja, sare moja na kupoteza moja, ikiwa katika nafasi ya saba. 
chanzo: http://www.globalpublishers.info

0 comments:

Post a Comment