Pages

Saturday 2 March 2013

Ngassa awa gumzo Angola

Winga wa Simba na timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Mrisho Ngassa alikuwa gumzo kwa mashabiki wa soka na waandishi wa habari nchini Angola baada ya Simba kutua nchini humo jana kwa ajili ya mechi yao ya marudiano ya michuano Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Recreativo de Libolo itakayochezwa kesho.

Akizungumza na NIPASHE akiwa Angola jana, kiongozi wa msafara wa Simba, Zacharia Hans Poppe alisema kuwa timu yao ilipokewa vyema na wenyeji wao huku Ngassa akifuatwa na watu wengi wakiwamo waandishi wa habari waliohitaji kufanya mahojiano naye.

Hans Poppe alisema kuwa Simba imeweka kambi kwenye mji wa Calulo ambao mechi yao ya kesho itachezwa kwenye uwanja Estadio Municipal de Calulo.

"Tumepokewa vizuri, kwa sasa (jana jioni) tujko kwenye kambi yetu mjini Calulo. Ni umbali wa dakika 35 kwa ndege kutoka mji mkuu wa Angola, (Luanda)," alisema Hans Poppe.

Aidha, kiongozi huyo wa msafara wa mabingwa hao wa Tanzanioa Bara alisema kuwa mchezaji Haruna Moshi 'Boban' anaywesumbuliwa na Malaria na kocha Mosses Basena ambaye jana alilazimika kwenda Uganda kumuuguza mke wake, wameachwa katika safari hiyo.

Katika mechi yao ya kwanza iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Februari 17, Simba wanaonolewa na kocha Mafaransa Patrick Liewig, walikubali kichapo cha goli 1-0.

Ngassa amekuwa akiwania na klabu kadhaa za nje ya Tanzania ikiwamo klabu ya El- Merreikh ya Sudan ambayo alitosa ofa yake. Alifunga goli liliyoipa ushindi wa 1-0 Taifa Stars katika mechi ya kimatiafa ya kirafiki dhidi ya Zambia Desemba 22 mwaka jana.
chanzo:nipashe

0 comments:

Post a Comment